Waziri Mkuu Majaliwa ameshiriki hafla ya Iftari na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza benki ya NMB kwa kuiunga mkono Serikali kwa kuisaidia jamii ikiwemo watoto wanaoishi katika mazingira magumu. “Kwa kufanya hivi mnapata thawabu kwa kuyagusa maisha ya jamii yenye uhitaji na kuwafanya wajione wenye thamani sawa na wengine. Ninatambua kuwa licha ya kuwakumbuka Watoto wenye uhitaji, mmekuwa mkichangia mahitaji muhimu kwenye shule